Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 30 May 2013

CUF yajipanga ‘kufufuka’ upya

                                      20Rajab,1434 Hijiriyah/ May 30,2013 Miyladiyah
 Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, kimejipanga kuhakikisha kinafanya kampeni  kuhamasisha wananchi wanajiunga nacho  kuanzia ngazi ya kijiji.
Akizungumza baada ya kikao cha kutathmini mafanikio ya mradi wa maendeleo, Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, Mbarala Maharagande alisema chama hicho kinajipanga kwa uchaguzi mkuu ujao.
Maharagande alisema CUF haitaki kurejea tena makosa ya kupoteza majimbo ambayo yalionyesha kuwa chini ya chama hicho, hivyo kitaanzisha mafunzo kwa viongozi wake wakiwamo madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Alisema mbinu hiyo inaratibiwa na uongozi wa juu wa taifa wa chama hicho, kila kiongozi mwenye dhamana anatakiwa kuhakikisha eneo lake linakuwa chini ya  CUF.
“CUF kinavyoungwa mkono na Watanzania hivi sasa tunajipanga  kweli hakuna kulala tena, uchaguzi mkuu upo mbele yetu wenzetu wakae chonjo,” alisema Maharagande.
Kuhusu mafanikio ya mradi wa maendeleo wa chama hicho unaofadhiliwa na Redicale, Maharagande alisema wameibua kero nyingi na kujionea migogoro ya kupandikizwa.
Alisema Serikali ndiyo inayokaribisha umaskini wakati  nchi imejaa utajiri, hivyo kuwashauri wananchi kubadilisha mwelekeo kwa kuchagua CUF.
Alisema nchi ina rasilimali nyingi ya gesi, mafuta na madini kitu ambacho kinatosha Serikali kutekeleza miradi yake bila kutegemea wafadhili.
Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa Mradi wa CUF/RV Mkoa wa Tanga, Mussa Mbarouk, alitaka Serikali kutekeleza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

0 comments:

Post a Comment