Bunge la Zimbabwe hapo jana Alhamisi liliidhinisha rasimu ya katiba mpya
baada ya mjadala mkali wa siku mbili. Wabunge 156 waliipigia kura ya
ndio huku idadi ndogo ikiipinga rasimu hiyo ya katiba mpya. Kwa mujibu
wa sheria za bunge, muswada wowote unahitaji thuluthi mbili au kura 140
kuweza kupita. Sasa rasimu hiyo iliyopitishwa kwa wingi wa kura kwenye
kura ya maoni mwezi Machi, itapelekwa kwenye bunge la Senet ambako
inatarajiwa kupitishwa na kisha baadaye Rais Robert Mugabe atatia saini
ili iwe sheria. Chama cha rais Mugabe cha ZANU-PF kimewalaumu wabunge wa
MDC kwa kujaribu kuchelewesha kuidhinishwa rasimu hiyo ya katiba ili
uchaguzi mkuu pia uchelewe kufanyika. Katiba mpya ni miongoni mwa
masharti muhimu yaliyotolewa na jamii ya kimataifa kwa ajili ya
kufanyika uchaguzi huru nchini Zimbabwe.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment