Kamati ya bunge la Kenya inayohusika na kuwachunguza watu wanaoteuliwa
kushika nyadhifa serikalini imeanza kazi ya kuwasaili mawaziri 16
waliopendekezwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto majuma
mawili yaliyopita. Leo alhamisi, kamati hiyo imewasaili mawaziri 5 kati
ya 16 na zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hadi Jumamosi. Kamati hiyo
inayoongozwa na spika wa bunge, Justin Muturi imefanya usaili huo mbele
ya vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa KICC.
Miongoni mwa waliosailiwa ni pamoja na Bi. Amina Mohammed ambaye
amependekezwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Henry Roticha (Fedha),
Anne Waiguru (Ugatuzi), Raychelle Omamo (Ulinzi) na Jacob Kaimenyi
(Elimu, Sayansi na Teknolojia). Iwapo mawaziri hao 16 wataidhinishwa na
kamati hiyo ya bunge, majina yao yatawasilishwa bungeni ili wabunge wote
wawapigie kura.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment