Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 15 April 2013

Zaidan ataka ushirikiano wa nchi za Kiafrika

 
Waziri Mkuu wa Libya ameziomba nchi za Kiafrika zitoe mashirikiano kwa nchi hiyo ili kuwezesha kurejeshwa fedha za Libya zilizoibiwa. Ali Zaidan Waziri Mkuu wa Libya ameziomba nchi za Kiafrika kushirikiana ili kufanikisha kurejeshwa fedha za Libya zilizoibiwa na kuwakabidhi  watu wa karibu wa Kanali Muammar Gaddafi kiongozi wa zamani wa Libya aliyeng'olewa madarakani wanaosakwa na serikali. Waziri Mkuu wa Libya pia amesema vitega uchumi vya nchi hiyo vilivyoko katika nchi za Kiafrika ni miongoni mwa mali za raia wa Libya na kuzitaka nchi za Kiafrika kuzilinda mali hizo.

0 comments:

Post a Comment