Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 15 April 2013

Mapigano mapya yazuka Jamhuri ya Afrika ya Kati

Watu wasiopungua saba jana waliuawa huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mapigano makali kati ya vikosi vilivyotwaa madaraka mwezi uliopita na wanamgambo vijana watiifu kwa rais waliyempindua madarakani nchini humo. Jenerali Moussa Dhaffane ambaye amesema amekuwa akikaimu nafasi ya msemaji wa serikali ameeleza kuwa mapigano ya jana yalianza baada ya vikosi viliyotwaa madarakani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kupiga doria katika ngome ya wapiganaji watiifu kwa Francois Bozize ambao walipatiwa silaha wakati waasi wa Seleka waliposonga mbele kuelekea mji mkuu Bangui. Mkuu wa Hospitali ya Bangui amesema kuwa watu saba waliuawa katika mapigano ya jana na kwamba idadi ya majeruhi inaongezeka kwa kuwa majeruhi wengine wanaendelea kufikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

0 comments:

Post a Comment