Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 15 April 2013

Maduro ashinda uchaguzi wa rais Venezuela

Tume ya Uchaguzi ya Venezuela imemtangaza Nicolas Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika jana nchini humo. Maduro amepata asilimia 50.66 ya kura huku mpinzani wake Henrique Capriles akipata asilimia 49.06. Capriles amepinga matokeo hayo ya uchaguzi. Tume ya Uchaguzi ya Venezula leo imeripoti kuwa zaidi ya asilimia 99 ya kura zimehesabiwa hadi sasa na kwamba matokeo ya uchaguzi hayawezi kubadilika. Nicolas Maduro amesema amepata ushindi halali na wa kikatiba.
Maduro ameahidi katika uongozi wake kuendeleza sera za kisoshalisti za kiongozi aliyemtangulia marehemu Hugo Chavez.

 

0 comments:

Post a Comment