Benki ya Dunia imesema kwenye ripoti yake mpya kuwa, uharamia wa
baharini nchini Somalia umesababisha kuongezeka gharama ya kuendesha
biashara ya kimataifa kwa zaidi ya dola bilioni 18 kila mwaka. Ripoti
hiyo aidha imesisitiza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa muhimu pia
umesababishwa kwa kiwango fulani na tatizo la uharamia wa baharini
katika pwani ya Somalia. Hata hivyo, Benki ya Dunia imekiri kwamba
uharamia umepungua mno katika kipindi cha miaka 2 iliyopita. Imesema
mafanikio hayo yametokana na juhudi za nchi mbalimbali kupeleka
wanajeshi wa majini kupiga doria katika maji ya kimataifa karibu na
pwani za Somalia na Aden. Mwaka 2009 zaidi ya meli 100 zilitekwa nyara
na maharamia huko Somalia jambo lililotoa pigo kubwa kwa biashara ya
mafuta na matunda katika soko la kimataifa.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment