Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 11 April 2013

Dk. Mwinyi azindua baraza

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amesema katika miaka ya karibuni matatizo ya kitaalamu yamekuwa yakitolewa uamuzi bila kuzingatia taratibu.
Dk. Mwinyi alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizindua Baraza la Usajili wa Wataalamu wa Afya ya Mazingira nchini.
Alisema hali hiyo ndiyo ilisababisha baraza hilo kuanzishwa kama chombo pekee cha kusimamia na kudhibiti utendaji wa maofisa afya ya mazingira nchini.
“Nchi zinazoendelea hivi leo zinakabiliwa na changamoto ya teknolojia endelevu, vitendea kazi duni, mazingira duni yasiyoridhisha kiafya, hali mbaya ya uchumi, soko la ajira, uzembe na uzururaji, ushindani wa kitaaluma, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na sekta ya kilimo na chakula,” alisema.
Kwa mujibu wa Waziri Mwinyi, katika sekta ya afya na ustawi wa jamii kuna changamoto nyingi zikiwemo za ongezeko la milipuko ya magonjwa kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Msajili wa Baraza la Afya ya Mazingira, Iddi Hoyange alisema taaluma ya afya ya mazingira ni muhimu kwa kuwa kazi yake kuu ni kuhakikisha jamii inashirikishwa kikamilifu katika suala zima la udhibiti na uzuiaji magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.
 

0 comments:

Post a Comment