Kiongozi wa kundi la waasi la Boko Haram nchini Nigeria, Abubakar Shekau
amesema kundi hilo halihitaji msamaha wa serikali na kwamba
litaendeleza mapambano dhdi ya kile alichokiita uchafu wa Wamagharibi.
Shekau amesema serikali ndiyo inayopaswa kuliomba msamaha kundi hilo.
Pia ametoa orodha ndefu ya jinai anazodai serikali imewatendea Waislamu
wa Nigeria. Hii ni katika hali ambayo, serikali ya Nigeria imetangaza
kuwa iko tayari kutoa msamaha kwa wanachama wa Boko Haram ambao wako
tayari kusitisha mashambulizi yao dhidi ya maafisa wa usalama pamoja na
raia nchini humo. Mpango huo wa msamaha umeratibiwa na viongozi wa
Kiislamu kutoka maeneo ya kaskazini mwa Nigeria ambao wamedai kwamba
wahanga wakubwa wa hujuma za Boko Haram ni Waislamu wenyewe. Hata hivyo
wanasiasa wa kusini mwa nchi wameijia juu serikali wakiitaka kutumia
mkono wa chuma kukabiliana na kundi hilo ambalo limetangaza hadharani
mfungamano wake na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment