Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 18 April 2013

Watu wanne wafa kwa kuangukiwa na nyumba

Watu wanne wamekufa baada ya kuangukiwa na nyumba kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humu katika Mkoa wa Singida.

Mbali ya watu hao, pia mifugo 14 ya aina mbalimbali imekufa pamoja na kuharibu ekari 1,119 za mazao mbalimbali na kuangusha nyumba 714 zikiwamo za tembe 543 na za bati 171.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Hezron Msule, madhara hayo yametokea katika kipindi cha wiki moja ya kwanza ya mwezi huu.

Msule aliyasema hayo ofisini kwake juzi alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya hali halisi ya madhara yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Mkalama.

Alisema idadi ya vifo na uharibifu wa mali na nyumba inaweza kuongezeka kwani bado wanaendelea kupokea taarifa kutoka kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Hata hivyo, alisema idadi kamili ya watu waliokosa mahali pa kuishi na hasara iliyopatikana, bado haijafahamika.

Aidha, alitoa wito kwa maafisa watendaji wa kata kutembelea kwenye maeneo yao ili wapate takwimu sahihi za waathirika wa mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa.

0 comments:

Post a Comment