Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 18 April 2013

Zuma: Afrika Kusini haitishwi na waasi wa Kongo DRC


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa, majeshi ya nchi yake hayaogopi vitisho vinavyotolewa na waasi wa M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baada ya Afrika Kusini kutangaza kwamba imepeleka wanajeshi wake kwenye kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Kongo, waasi wa M23 wametishia kufanya mashabulizi makali dhidi ya wanajeshi wa Afrika Kusini.
Mwezi uliopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutumwa kikosi maalumu cha wanajeshi 2,500 huko mashariki mwa Kongo kwa shabaha ya kukabiliana na waasi hao.
Wakati huohuo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kikosi kilichopewa mafunzo na Marekani nchini Kongo kinatuhumiwa kufanya vitendo vya ubakaji na kuwadhalilisha wanawake. Haja Zainab Hawa Bangura ambaye ni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ukatili wa kijinsia amesema kuwa, jumla ya wanajeshi 33 wakiwemo maafisa kadhaa watafunguliwa mashtaka hivi karibuni kwa tuhuma za kufanya vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake wa Kongo. Bangura amesema kuwa, wanawake wasiopungua 126 walibakwa mwezi Novemba mwaka jana mashariki mwa Kongo.

0 comments:

Post a Comment