Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 6 April 2013

Watu 8 wauawa katika machafuko Misri


                              26,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 07,2013Miyladiyah

Nchini Misri watu zaidi ya wanane wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mapigano baina ya Wakristo na Waislamu karibu na mji mkuu Cairo.
Televisheni ya Press TV imenukulu maafisa wa usalama wakisema kuwa Mwislamu na Wakopti saba waliuawa Ijumaa usiku baada ya familia mbili kufyatuliana risasi katika mji wa al-Khusus mkoani Qalyubiyah yapata kilomita 12 kaskazini magharibi mwa Cairo.
Watu zaidi ya 20 walijeruhiwa katika tukio hilo. Duru zinasema machafuko hayo yalianza baada ya vijana wachochezi wa pote la Kikristo la Kopti kuanza kuchora misalaba katika kuta za jengo la taasisi moja ya Kiislamu mjini humo. Maafisa wa usalama wamefanikiwa kudhibiti hali ya mambo.
Hii si mara ya kwanza kuibuka mapigano baina ya Waislamu wa Misri na Wakristo wa pote la Kopti. Inakadiriwa kuwa Wakopti ni asilimia 10 ya watu milioni 83 nchini Misri.

0 comments:

Post a Comment