Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 6 April 2013

UN: Mauaji ya kimbari Rwanda ni funzo


                              26,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 07,2013Miyladiyah
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa salamu kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 19 tangu yajiri mauaji ya kimbari nchini Rwanda na kusema yaliyotokea nchini humo ni funzo na kwamba ofisi yake inachukua hatua kila siku kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena. Bw.Ban ametoa mfano na kusema mshauri wake anayehusika na hatua za kuepusha mauaji ya kimbari, anafuatilia viashiria vyovyote vile duniani vinavyoweza kuwa chanzo cha tukio kama la Rwanda.  Amesema wajibu wa kulinda binadamu kwa sasa umekuwa ndio kanuni ya kimataifa na kwamba pamoja na hatua hizo, Umoja wa Mataifa unahakikisha wale wote wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari hawakwepi mkono wa sheria. Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepongeza Rwanda kwa mwelekeo mpya baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Ameisihi serikali na wananchi wa Rwanda kuendeleza moyo wa utengamano, maridhiano na ujenzi wa taifa. Aprili 7 kila mwaka huwa mwanzo wa siku 100 za kukumbuka mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda  ambapo takribani watu milioni moja waliuawa

0 comments:

Post a Comment