Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 6 April 2013

Wanafunzi 1,605 hawajaripoti sekondari


                              26,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 07,2013Miyladiyah

JUMLA ya wanafunzi 1,605 miongoni mwa 4,604 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wameshindwa kuripoti kwenye shule za sekondari walizopangiwa.
Ofisa Elimu anayeshughulikia elimu ya sekondari wilayani Urambo, Grace Monge, aliitaja idadi ya wanafunzi walioingia kidato cha kwanza mwaka huu kuwa ni 1,605.
Alisema kati ya wanafunzi hao 1,605 wavulana ni 800 na wasichana ni 805. Walioripoti mpaka sasa ni 2,989, wavulana 1,713 na wasichana 1,276.
Kwa maelezo yake, idadi hiyo ya watoto walioshindwa kuripoti ni kubwa ikilinganishwa na mikakati waliyokuwa wamejiwekea.
Alitaja sababu zilizochangia wanafunzi hao kushindwa kuripoti shuleni ni baadhi yao kuolewa mapema, kukosa ada na mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni ikiwamo sare za shule na vifaa vya shule kwa ujumla.
Pia alisema kitendo cha wazazi kuwatumikisha watoto wao katika shughuli za kilimo na wazazi wengine kuwazuia watoto wao kuendelea na masomo kwa kisingizio cha kupoteza nguvu kazi katika kilimo hicho kumechangia hali hiyo.
Alisema halmashauri ya wilaya hiyo imekusudia kuwasaka na kuwafungulia mashitaka wazazi wote waliowazuia watoto wao kujiunga na wenzao sambamba na kuwaelimisha wazazi hao juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto na madhara ya kumkosesha haki hiyo ya msingi.
Naye Coleta Hassan, ambaye ni Ofisa Elimu Maalumu Idara ya Msingi, akizungumzia mikakati iliyowekwa na halmashauri hiyo katika suala la kuboresha elimu, alisema kuwa wamekusudia kukarabati madarasa, ofisi, nyumba za walimu, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wazazi kuchangia chakula ili kuanzisha utaratibu wa kuwapatia chakula cha mchana wanafunzi wote wanapokuwa shuleni.

"Chanzo cha habari hii ni Tanzania Daima"

0 comments:

Post a Comment