Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 29 April 2013

Wakazi wa Kordofan wapinga mashambulizi ya waasiWananchi wa Kordofan kaskazini nchini Sudan, wamefanya maandamano ya kupinga mashambulizi ya waasi jimboni hapo. Maandamano hayo yalifanyika hapo jana Jumapili katika eneo la Umm Ruwaba wakipinga mashambulizi yanayofanywa na waasi waHarakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Sudan (SPLA) tawi la kaskazini mwa Sudan. Waandamanaji pia walitoa nara wakiitaka serikali ya Khartoum kuchukua hatua kali dhidi ya waasi nchini humo. Siku ya Jumamosi Msemaji wa jeshi la Sudan al- Sawarmi Khalid aliwambia waandishi wa habari kuwa, jeshi la Sudan lilikuwa limeanzisha msako mkali katika eneo hilo la Umm Ruwaba baada ya kuwafurusha waasi wa(SPLA) tawi la kaskazini waliokuwa wamevamia eneo hilo. Mashambulizi ya waasi hao yalijiri saa chache baada ya kutangazwa kuvunjika mazungumzo ya serikali ya Khartoum na ujumbe wa harakati hiyo yaliyokuwa yakifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya usimamizi wa Thabo Mbeki mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya amani ya Sudan.

0 comments:

Post a Comment