Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan ametangaza kuwa, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Libya imenusurika kushambuliwa na watu wenye silaha. Zeidan
amesema hayo katika kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, watu
wenye silaha waliivamia wizara hiyo kwa lengo la kuishambulia lakini
polisi walifanikiwa kuzima haraka jaribio hilo la shambulizi. Aidha
waziri mkuu huyo wa Libya ameongeza kuwa, watu wenye silaha pia walikuwa
wamepanga kutekeleza shambulizi jingine dhidi ya jengo la idara ya
habari ya Libya na kwamba, shambulizi hilo limezimwa kwa juhudi za
polisi wa nchi hiyo. Ali Zeidan amesisitiza kuwa, serikali ya Libya iko
makini dhidi ya mashambulizi kama hayo na kwamba, haitorudi nyuma katika
mapambano yake dhidi ya wahalifu na watu wanaotaka kuhatarisha usalama
wa nchi hiyo. Kabla ya hapo siku ya Jumapili pia ilikuwa imetangazwa
kuwa, kundi la watu wenye silaha lilikuwa lilizingira jengo la Wizara ya
Mashauri ya Nje ya nchi hiyo. Viongozi wa serikali ya sasa ya Libya
wametakiwa kuzima harakati za wafuasi wa utawala uliong'olewa
madarakani nchini humo ili kuepusha matukio kama hayo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment