Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 29 April 2013

Tunisia: An Nahdha itafungamana na mfumo Bunge Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya an-Nahdha ya Tunisia, Dakta Rashid al Ghanushi amesisitizia juu ya kufungamana harakati hiyo na mfumo wa uwiano wa bunge nchini humo. Al Ghanushi amesisitiza kuwa, harakati ya an-Nahdha inasisitiza juu ya kuwepo mfumo wa uwiano wa bunge ambao kwa mujibu wake kutakuwepo makubaliano juu ya mamlaka na majukumu  ya rais na waziri mkuu wa nchi. Aidha amesisitiza kuwa, lengo la an-Nahdha katika kuimarisha mfumo huo wa bunge ni kwa ajili ya kukabiliana na mfumo wa udikteta. Hivi karibuni viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda serikali ya Tunisia, walijadiliana kuhusiana na mfumo wa kisiasa wa hapo baadaye wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na wadhifa wa rais na waziri mkuu wa nchi. Hata hivyo mazungumzo hayo hayajakuwa na natija mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment