Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 6 April 2013

Tanzania yamtaka Rais wa Malawi aache kutapatapa                              25,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 06,2013Miyladiyah
 Serikali ya Tanzania imeitaka Malawi iache kutoa maneno yasiyo na msingi kuhusiana na mgogoro wa mipaka wa Ziwa Nyasa. Kauli hiyo rasmi ya serikali ya Tanzania imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bernard  Membe na imekuja baada ya Rais Joyce Banda wa Malawi kutangaza katika  baadhi ya vyombo vya  habari  kuwa atapeleka  suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). Membe amesema, Malawi inatakiwa isubiri uamuzi wa jopo la usuluhishi lifanye kazi na litoe maamuzi yake. Aidha serikali ya Tanzania imekanusha madai kupelekewa nyaraka za siri kutoka kwa katibu wa jopo hilo na kusema madai hayo hayana msingi. Kabla ya hapo Rais wa Malawi alikuwa ameituhumu Tanzania kuwa, kuna Mtanzania anayeitwa John Tesha ametoa  habari za siri na kuiba nyaraka za siri kutoka katika jopo hilo na kuikabidhi serikali ya Tanzania. Akilitolea ufafanuzi   jambo hili, Waziri Membe amesema kuwa, Tanzania na jopo hilo   limestushwa na madai hayo ya Rais wa Malawi. Membe aidha amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali ya  Malawi inapaswa iache kutapatapa mara Uingereza, mara Marekani, mara kwa Jumuia ya Madola na mara kwa Umoja wa Afrika (AU) na kuonana viongozi mbalimbali wa dunia, bali iamini kuwa jopo la Mzee Chissano linaweza kutatua tatizo hilo

0 comments:

Post a Comment