Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 6 April 2013

Sisitizo la Haniya la kutoutambua utawala wa Kizayuni                              25,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 06,2013Miyladiyah
 Ismail Haniya Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina inayoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesisitiza kuwa, Hamas  kamwe haitautambua utawala bandia wa Israel. Haniya amesema kuwa, misimamo ya Hamas tokea ilipoanzishwa miaka 25 iliyopita iko wazi kwamba haiutambui rasmi utawala ghasibu wa Israel na wala hawakubaliani  na masharti yaliyotolewa na kamati ya pande nne yaani Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na Russia wa kuutambua utawala huo bandia wa Israel. Kamati hiyo iliitaka harakati ya Hamas kuutambua utawala wa Israel na kujiepusha na utumiaji silaha dhidi ya Wazayuni. Ameongeza kuwa, hali ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za Wazayuni ni mbaya mno na kusisitiza kuwa, pamoja na kuendelezwa jinai dhidi ya binadamu, jinai za kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu na wafungwa wa Kipalestina kwenye jela za Wazayuni, wananchi wa Palestina wataendeleza mbele mapambano yao na wala hawatasalimu amri mbele ya ukandamizaji  wa utawala wa Israel.

0 comments:

Post a Comment