Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 6 April 2013

Jenerali wa Kimarekani atimuliwa kazi kwa ubakaji                              25,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 06,2013Miyladiyah
Wizara ya Ulinzi ya Marekani 'Pentagon' imemfuta kazi Meja Jenerali Ralph Baker Kamanda wa Majeshi ya Marekani katika eneo la  Mashariki  na Pembe ya Afrika baada ya kukumbwa na kashfa ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia barani humo.  Meja Robert Freeman Msemaji wa Pentagon amesema kuwa, Meja Jenerali Baker ambaye alikuwa akiviongoza vikosi vya Marekani  katika eneo hilo lenye makao yake  nchini Djibouti, ametimuliwa baada ya Jenerali Carter Ham  Kamanda wa Vikosi vya Marekani barani Afrika AFRICOM kutoa amri hiyo. Jenerali Carter Ham alitoa amri hiyo wakati ulipokuwa  umesalia muda mchache  kabla ya kumkabidhi  hapo jana Jenerali David Rodriguez  ukamanda wa vikosi vya Marekani barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment