21Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ May 01,2013 Miyladiyah
Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan ametoa msamaha kwa askari ambao hivi
karibuni walikula njama za kufanya mapinduzi dhidi ya serikali ya nchi
hiyo. Rais al Bashir ametoa msamaha kwa askari saba wa idara ya usalama
na ulinzi wa taifa ya Sudan ambao walitiwa mbaroni baada ya kutuhumiwa
kula njama za kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani nchini humo.
Kwa mujibu wa habari hiyo, msahama huo umetolewa baada ya askari hao
kuomba radhi kwa Rais al Bashir hivi karibuni. Itakumbukwa kuwa wiki
kadhaa zilizopita Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan alitoa msamaha kwa
kiongozi mmoja nchini humo aliyetiwa mbaroni kwa tuhuma za kupanga
njama kama hizo sambamba na kuwahukumu kifungo cha miaka miwili hadi
minane watuhumiwa wengine sita wa kesi hiyo. Weledi wa masuala ya
kisiasa waliutaja msamaha huo kuwa mwanzo wa kuelekea kwenye maelewano
ya kisiasa nchini Sudan.
0 comments:
Post a Comment