Misri imejiondoa katika mazungumzo ya Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na
Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) unaoendelea huko Geneva Uswisi
ukilalamikia kushindwa jamii ya kimataifa kutekeleza azimio la kulifanya
eneo la Mashariki ya Kati lisiwe na silaha hata moja ya nyuklia. Leo
Jumatatu Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetoa taarifa na kueleza kuwa
Cairo imeamua kuacha kushiriki katika mazungumzo hayo ya wiki mbili
kufuatia kushindwa nchi nyingine kutekeleza azimio la mwaka 1995
linalotaka kuhakikisha kuwa eneo la Mashariki ya Kati halina silaha za
nyuklia. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imeeleza kuwa Cairo
haiwezi kusubiri milele utekelazaji wa uamuzi huo. Wizara ya Mambo ya
Nje ya Misri imesema kuwa hatua ya nchi hiyo ya kusitisha kushiriki
kwenye mkutano wa Geneva ni sawa na kutuma ujumbe mzito kwamba Cairo
haikubaliani na hatua ya jamii ya kimataifa ya kutolipa uzito suala la
kuangamizwa silaha za nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Itakumbukwa kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndilo dola pekee
linalomiliki silaha za nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati na hadi
leo unakaidi mashinikizo ya jamii ya kimataifa ya kuruhusu wakaguzi wa
nyuklia kutembelea vinu vyake vya nyuklia.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment