Kwa mara nyingine mahakama ya kijeshi nchini Tunisia imemuhukumu dikteta
wa nchi hiyo aliyekimbia nchi kifungo cha maisha jela bila ya kuwepo
mahakamani. Hii ni mara ya tatu kwa mahakama hiyo ya kijeshi nchini
Tunisia kumuhukumu dikteta Zainul Abidin Bin Ali kwa makosa ya mauaji
dhidi ya wananchi katika harakati za mapinduzi ya wananchi za mwaka 2010
na 2011. Wakati huo huo Rafik Haj Kassem, Waziri wa Mambo ya Ndani wa
utawala wa Bin Ali, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela huku Ali
Saryati, Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama ya Tunisia akifutiwa tuhuma
zote zilizokuwa inamkabili. Inasemekana kwamba, familia ambayo
ilimpoteza mtu mmoja au kujeruhiwa watu wawili wa familia hiyo katika
harakati za mapinduzi hayo, italipwa kuanzia Dinar elfu 12 hadi laki
moja sarafu ya Tunisia, sawa na Dola za Kimarekani elfu nane hadi elfu
sabini.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment