Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday 15 April 2013

Sudan kuheshimu makubaliano na Sudan Kusini

Makamu wa Rais wa Sudan amesisitiza kuwa nchi yake inaheshimu na kusisitiza kutekelezwa makuablaino ya ushirikiano iliyofikia na jirani yake Sudan Kusini. Nafi Ali Nafi Makamu wa Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesisitiza kuwa Sudan itaheshimu kikamilifu makubaliano ya ushirikiano iliyosaini na serikali ya Sudan Kusini.
Makamu wa Rais wa Sudan ameyataja mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Kadukali makao makuu ya mkoa wa Korofani Kusini kuwa ni njama za baadhi ya pande za kutaka kuvunja makubaliano hayo na kwamba mapatano hayo yataendelea kudumu licha ya njama hizo. Nafi Ali Nafi pia ameyataka makundi yote ya kisiasa ya Sudan kuungana na kujiweka mbali na maadui na kuongeza kuwa Sudan itaendelea kuijenga upya nchi hiyo ili kutimiza matarajio ya wananchi.
 

0 comments:

Post a Comment