Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 15 April 2013

Serikali yadaiwa kuvunja haki za wazeeMTANDAO wa Kinga Jamii Tanzania (TSPN) umeishambulia serikali kwa madai kuwa imekuwa kinara wa kuvunja haki za wazee ikiwemo kushindwa kulinda haki zao za kuishi.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Katibu Mkuu wa TSPN Isaka Msigwa, alisema serikali imeshindwa kulinda haki za kuishi, kwani badala ya mauaji ya wazee kupungua yanaongezeka.
“Mauaji ya wazee yanashika kasi kubwa na yanatisha kutokana na kutuhumiana kwa uchawi ama kutaka kuwapora mali zao bila kuwepo kwa juhudi zozote za kupambana na mauaji hayo.
“Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu 2011, inaonesha mauaji yameongezeka kutoka 579 mwaka 2010 hadi 642 mwaka 2011, hali inayosikitisha kuona mauaji yakiongezeka badala ya kupungua,” alisema Msigwa.
Alisema kuwa mtandao huo unahitaji serikali itoe taarifa kwa umma juu ya ripoti ya hatua zilizofikiwa kuhusu mauaji ya wazee.

Aidha, alisema serikali bado haijawatendea haki wazee kwani wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja kushindwa kuwalipa pensheni bila kujali kuwa walikuwa wanafanya kazi ama la.

“Inashangaza kuona baadhi ya nchi zenye uchumi mdogo
kama Mauritius ambayo inategemea miwa inaweza kuwalipa wazee zaidi ya sh 300,000 kila mwezi wakati Tanzania yenye uchumi mkubwa kama vile madini, mito, maziwa, vivutio kwa maana ya kuwa na watalii wengi, wanashindwa kuwalipa wazee pensheni ya kutosha,” alisema Msigwa.
 

0 comments:

Post a Comment