Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 15 April 2013

Harakati ya MEND yatishia kuanzisha mashambulizi


Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta (MEND) imetishia kuanzisha tena mashambulizi yake dhidi ya Misikiti, taasisi za Kiislamu na kuwauwa viongozi wa Kiislamu. Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta jana usiku ilitoao taarifa na kuwatishia Waislamu wa Nigeria kuwa itaishambulia misikiti, taasisi za Kiislamu, mikusanyko ya waumini wa Kiislamu katika maeneo matukufu na kuwauwa viongozi wa Kiislamu. Taraifa hiyo imeongeza kuwa mashambulizi dhidi ya misikit na vituo vya Kiislamu yataanza tarehe 30 mwezi ujao. Harakati ya Ukombozi ya Niger Delta huko nyuma ilitishia kuanzisha tena mashambulizi yake kama radiamali kwa hukumu ya kifungo cha miaka 24 jela iliyotolewa kwa Henry Okah kiongozi wa zamani wa kundi hilo na mahakama moja ya Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment