Imam wa msikiti wa al-Islam wa Washington Marekani amesema kuwa,
nchini Myanmar kunaendelea kushuhudiwa vita vya dunia dhidi ya Waislamu
huku Umoja wa Mataifa ukiendelea kunyamaza kimya. Sheikh Abdul Alim
Mussa amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya
Kimataifa ya Press TV kuwa, kuteswa Waislamu wa Myanmar ni sawa na "Vita
vya Dunia Dhidi ya Uislamu" na kwamba, Umoja wa Mataifa umeendelea
kunyamazia kimya jinai na mauaji dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Imamu
wa Msikiti wa al-Islam wa Washington Marekani amesema kuwa, Vita vya
Dunia dhidi ya Uislamu vinafanyika nchini Myanmar na kwamba, watu wasio
na hatia yoyote wanauawa kiholela huku vyombo vya habari vya Kimagharibi
vikinyamazia kimya jinai hizo dhidi ya binadamu. Tarehe 20 mwezi
uliopita wa Machi, zaidi ya Waislamu 40 waliuawa na misikiti kadhaa
kuchomwa moto katika miji kadhaa ya katikati mwa Myanmar. Weledi wa
mambo wanaamini kuwa, siasa za kindumilakuwili za Wamagharibi kuhusu
haki za binadamu na kulinda utu wa mwanadamu zimechangia katika mauaji
ya Waislamu wa Myanmar.
Na Salum Bendera
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment