Rais mstaafu wa awamu ya tatu nchini Tanzania Bwana Benjamin
Mkapaamewataka Watanzania kutotoa maoni kuhusiana na Katiba mpya kwa
misingi ya udini. Mkapa ameyasema hayo mjini Masasi ambapo ameliasa
taifa la Tanzania kujiepusha na utoaji maoni ya Katiba mpya kwa misingi
ya dini. Mkapa amesema Katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za kidini
kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa. Rais huyo mstaafu wa Tanzania
amesema kama ninavyomnukuu “Wapo watakaopata uwakilishi kupitia rasimu
ya Katiba ya nchi. Namwomba Mwenyezi Mungu awape mwanga, muhakikishe
jambo moja tu ambalo litakuwa msingi mkubwa wa amani na maendeleo na
umoja wa taifa letu. Watupatie Katiba ambayo inatoa fursa kamilifu ya
kila mtu kuwa na imani yake.“ Mwisho wa kunukuu. Vilevile rais huyo
mstaafu wa Tanzania amesisitizia juu ya nchi hiyo kuepukana na imani
moja rasmi kama ambavyo nchi hiyo haina kabila moja.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment