Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 1 April 2013

Wahanga wa kuporomoka ghorofa Dar wafikia 34

Idadi ya viwiviwili vya watu waliokufa kwa kuporomokewa na jengo la ghorofa jijini Dar es Salaam Tanzania imefikia 34 huku shughuli ya kutafuta maiti nyingine ikiendelea, zikiwa zimepita siku tatu tangu ilipotokea ajali hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki amenukuliwa akisema kuwa, miili mingine kumi imepatikana baina ya jana mchana na leo Alfajiri na hivyo kuifanya idadi ya watu waliopoteza maisha yao na ambao wamepatikana hadi sasa kufikia 34. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 60 mpaka 70 walikuwa katika jengo hilo la ghorofa kumi na sita lililoporomoka siku ya Ijumaa. Wakati huo huo, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema matukio mengi mabaya kama hayo nchini yamekuwa yakisababishwa na mafisadi wasiojali maisha ya wengine. alitoa kauli hiyo alipotembelea eneo la ajali kuwapa pole wafiwa waliopoteza ndugu zao, akisema kama sheria na kanuni za ujenzi zingezingatiwa tukio hilo lisingetokea. Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete jana aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuwafariji.

0 comments:

Post a Comment