Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 7 April 2013

Mkutano wa kusaidia Darfur waendelea Doha Qatar


                                    27Jumaadal ula,1434 Hijiriyah/ April 08,2013 Miyladiyah
 Wawakilishi wa nchi wahisani na mashirika ya utoaji misaada wanaendelea kukutana katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kwa shabaha ya kuunga mkono mkakati wa kuchangisha mabilioni ya dola kwa ajili ya kulijenga upya jimbo la Darfur la Sudan baada ya mzozo wa muongo mmoja. Kiongozi wa ujumbe wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Jorg Kuhnel amesema mkutano huo ni fursa ya kipekee kwa Sudan na kubadilisha hatma ya jimbo hilo lililokumbwa na hali ya mchafukoge. Taarifa kutoka Doha Qatar zinasema kuwa, mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa na wajumbe 400 kutoka maeneo mbalimbali na unafanyika kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Julai mwaka 2011, ambapo Sudan ilitiliana saini  na muungano wa makundi ya waasi mjini Doha. Duru za karibu na mkutano huo zinasema kuwa, mkutano huo unakusudia kukusanya Euro bilioni 5.5 ili kuutekeleza mpango wa miaka sita wa kulisaidia jimbo la Darfur.

0 comments:

Post a Comment