Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 30 April 2013

Mkutano: Ufisadi upigwe vita barani Afrika




Mkutano wa kupambana na ufisadi wa kiidara na kifedha barani Afrika umefanyika Kampala mji mkuu wa Uganda kwa wajumbe kusisitiza juu ya kutokomezwa ufisadi barani humo.
Washiriki wa mkutano huo wamesisitiza juu ya kuungwa mkono sheria ya kupambana na ufisadi ambayo inapaswa kutekelezwa kikamilifu katika nchi zote za Afrika. Mathew Opoku Prempeh, Mbunge wa Bunge la Ghana amesema kwenye mkutano huo kwamba, sheria pekee si hazitoshi, kwani katika baadhi ya nchi za Kiafrika kuna sheria nyingi dhidi ya vitendo hivyo lakini ufisadi unaendelea kukithiri kwenye nchi  hizo. Amesisitiza kuwa hatua za kivitendo zinapaswa kuchukuliwa kupiga vita ufisadi barani Afrika.
Washiriki wa kongamano hilo la Kampala wameafikiana kwamba serikali za bara la Afrika zitangaze utajiri wa viongozi wao wa ngazi mbalimbali

0 comments:

Post a Comment