Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 30 April 2013

Mwili wa Kilonzo kupasuliwa leo
Mwili wa aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Makueni nchini Kenya Mutula Kilonzo unatarajiwa kufanyiwa upasuaji leo baada ya shughuli hiyo kuakhirishwa jana.
Shughuli hiyo inafanyika ili kubaini sababu halisi ya kifo cha ghafla cha waziri huyo wa zamani wa elimu wa Kenya kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa nyumbani kwake.
Familia ya Kilonzo imemwajiri mwanapatholojia wa Uingereza kushiriki katika timu inayochunguza kifo cha mwanasiasa huyo aliyewahi kushika myadhifa mbalimbali za uwaziri katika serikali ya Kenya.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma wa Kenya Keriako Tobiko ameteua jopo la waendesha mashtaka kusaidia polisi katika uchunguzi wa kifo cha Mutula Kilonzo

0 comments:

Post a Comment