Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 21 April 2013

Mabrouk: Nauli za daladala bado ndogo

                               12Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 22,2013 Miyladiyah

WAKATI wananchi wakilalamika kupanda kwa nauli, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala, Sabri Mabrouk, amesema nauli hiyo bado ni ndogo.
Mabrouk alitoa kauli hiyo alipozungumza na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa wanaolalamika ni wale walioingia jijini huku wakiwa hawana shughuli maalumu za kufanya.
Alisema ugumu wa maisha haukusababishwa na kupanda kwa nauli bali ulikuwepo tangu utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika tawala mbalimbali zijazo.
“Kwa watu tulioishi pamoja katika maisha ya ugumu ugumu nikisema hivyo wananielewa, lakini najua wapo walionufaika kutokana na kuwa na jamaa ambao walikuwa viongozi katika serikali; hao labda ndio wanaweza kushindwa kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.
“Pia wananchi wajue kila kitu kizuri kina gharama zake, hivyo ili kuboresha huduma zetu za usafiri ni lazima wananchi wakubali kuchangia kile kinachostahili,” alisema Mabrouk.
Akizungumzia mfumo wa huduma ya usafirishaji jijini kuwa wa kampuni, Mabrouk alisema haukwepiki bali ni muhimu kwa wamiliki wa daladala kutumia fursa hiyo kujiunga na kuanzisha kampuni.

0 comments:

Post a Comment