Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 21 April 2013

Usafiri wa treni Dar kuanza leo

                        12Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 22,2013 Miyladiyah

UONGOZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umesema usafiri wa treni jijini Dar es Salaam utaanza tena leo baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na kuharibika kwa miundombonu.
Usafiri huo ulisitishwa kwa wiki tatu kuanzia Machi 24 mwaka huu kutokana na kuharibika kwa miundombinu kulikosababishwa na mvua.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Uhusiano wa shirika hilo, Midladjy Maez, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini,Kipallo Kisamfu, ilieleza kuanza tena kwa usafiri huo kunatokana na kukamilika kwa kazi ya ukarabati wa tuta lililoharibika eneo la Tabata Relini na Mwananchi.
“Wahandisi wa Kampuni Hodhi za Mali na Uendelezaji wa Miundombinu ya Reli (Rahco) walikabidhi eneo hilo kwa wahandisi wa TRL Aprili 19 mwaka huu.
“Pamoja na ukarabari huo kukamilika, ukarabati wa kuimarisha eneo hilo utaendelea kufanywa na Rahco,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
taarifa hiyo ilieleza kuwa hakuna mabadiliko ya nauli na kwamba kila abiria mtu mzima atatakiwa kulipia sh 400 na watoto na wanafunzi sh 100 kwa safari moja.

0 comments:

Post a Comment