Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 12 April 2013

Kesi ya Rupiah Banda yachukua sura mpya Zambia

Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda ana haki ya kwenda mahakamani kulalamikia kuondolewa kinga yake ya  kutoshtakiwa. Jaji wa Mahakama Kuu ya Zambia amesema kuwa, Banda ana haki ya kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na bunge la nchi hiyo ya kumuondolea kinga ya kutoshitakiwa. Mnamo tarehe 15 Machi mwaka huu, bunge la Zambia lilimuondolea kinga ya kutoshtakiwa Rupiah Banda ili apelekwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kufanya ubadhirifu katika kipindi cha miaka mitatu aliyokuwa madarakani. Rais wa zamani wa Zambia anakabiliwa na tuhuma hizo amma wafuasi wake wanaamini kwamba, Rais Michael Sata wa Zambia ndiye aliyepanga  njama hizo kwa lengo la kumdhoofisha kisiasa Rupiah Banda.

0 comments:

Post a Comment