Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 12 April 2013

Wanajeshi 5 wafariki ajali ya helikopta Mali

Wanajeshi watano  wa Mali wameuawa baada ya helkopta ya kijeshi waliyopanda kuanguka nchini humo. Jeshi la Mali limethibitisha kuanguka kwa helkopta hiyo na wanajeshi  wote watano waliokuwemo ndani ya chombo hicho kupoteza maisha. Taarifa ya Jeshi la Mali imeeleza kuwa, helkopta hiyo ilianguka jana katika eneo la Sevare kutokana na matatizo ya kiufundi. Hata hivyo jeshi la Mali limeeleza kuwa, litafanya uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo. Jeshi la Mali limetangaza kuanguka kwa helkopta hiyo, huku kukiwa na uvumi kwamba wanamgambo waasi ndio waliofanya shambulio la kuitungua helikopta hiyo.

0 comments:

Post a Comment