Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 24 April 2013

Jeshi la Kongo lapambana na waasi Kivu Kusini



Watu wasiopungua 20 wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na makundi ya waasi.
Duru za habari zimeripoti kuwa, mapigano hayo yametokea baada ya wanamgambo wa makundi mawili ya waasi kushambulia kituo kimoja cha jeshi kwenye eneo la Chishado katika mkoa wa Kivu Kusini. Ripoti zinasema kuwa, wengi kati ya wahanga wa mapigano hayo ni raia wa kawaida na waasi.
Wakati huo huo, jeshi la Kongo limethibitisha kutokea mapigano hayo na kusema kuwa yanaendelea na kwamba kuna wasiwasi idadi ya waliouawa itaongezeka. Walioshuhudia wanasema kuwa, vikosi vya jeshi la serikali vililazimika kuondoka katika kituo chao hicho baada ya kushambuliwa na waasi.
Haijajulikana ni kundi gani la waasi lililohusika kwenye mashambulizi hayo huko mashariki mwa Kongo DRC.

0 comments:

Post a Comment