Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 24 April 2013

Angola kupunguza ufa kati ya matajiri na masikini





Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Angola kupunguza tofauti kubwa iliyopo kati ya matajiri na masikini katika nchi hiyo inayopiga hatua za maendeleo kutokana na utajiri wa mafuta.
Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Luanda, Navi Pillay ameipongeza serikali ya Angola kwa hatua ilizopiga katika kukarabati miundombinu na kusafisha maelfu ya mabomu ya ardhini baada ya vita vya ndani vilivyodumu kwa miaka 27. Hata hivyo katika mazungumzo yake na  Rais Jose Eduardo Dos Santos, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, kuna umuhimu wa kupunguza tofauti kubwa iliyopo kati ya watu masikini na matajiri na kuboreshwa haki za binadamu.
Angola ambayo ni nchi ya pili inayozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika, imekuwa ikipiga hatua za maendeleo tangu vita vya ndani vilipoisha mwaka 2002. Hata hivyo vyama vya upinzani na makundi ya kutetea haki za binadamu yanamlaumu Rais Eduardo Do Santos kwamba hajachukua hatua za kupambana vilivyo na umasikini kwenye nchi hiyo

0 comments:

Post a Comment