Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 24 April 2013

Zaidi ya watu 100 wauawa nchini Iraq




Zaidi ya watu 100 wameuawa katika machafuko ya siku mbili yaliyotokea nchini Iraq baada ya kujiri mapigano kati ya askari jeshi na waandamanaji na pia watu wenye silaha katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa nchi hiyo. Machafuko hayo yalianza baada ya waandamanaji kwenye mji wa al Hawijah kuzusha fujo eti wakidai damu ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein. Serikali ya Iraq inasema kuwa, vujo na machafuko hayo yanasababishwa na mtandao wa al Qaida na wafuasi wa chama cha Baath kilichoondolewa madarakani.
Kwingineko watu 15 wameuawa na wengine 42 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kati ya vikosi vya jeshi la Iraq na wanamgambo wenye silaha kwenye mkoa wa Salahuddin ambapo wanamgambo hao walivamia vituo kadhaa vya upekuzi.


0 comments:

Post a Comment