Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 11 April 2013

Iran na Burundi zatiliana saini mikataba minane

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Burundi zimetiliana saini mikataba minane kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili.
Mikataba hiyo imetiwa saini hapa Tehran katika kikao kilichohudhuriwa na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Mikataba iliyotiwa saini inahusu ushirikiano katika uga wa kilimo, huduma ya utibabu wa mifugo, mafunzo ya kiufundi, afya, masomo ya tiba, biashara na kuondolewa viza.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliwasili Tehran siku ya Jumanne akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Iran na Burundi. Katika safari yake hapa nchini Rais wa Burundi pia alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mbali na kutembelea miradi kadhaa ya maendeleo.
Hatua za kuimarisha ushirikiano wa Iran na Burundi zinachukuliwa katika fremu ya siasa maalumu za Jamhuri ya Kiislamu za kuzipa kipaumbele maalumu nchi za Kiafrika pamoja na azma yake ya kuzidisha uhusiano na nchi hizo

0 comments:

Post a Comment