Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 11 April 2013

Mafuriko Kenya: 34 wafariki, 26,000 wabaki bila makao

Nchini Kenya mvua za masika zilizoanza mapema mwezi huu zimesababisha mafuriko makubwa. Watu 34 wamepoteza maisha na wengine elfu 26 wamebaki bila makao.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetoa taarifa na kusema vifo vimeripotiwa katika maeneo ya Nyakach na Homa Bay, Bura katika Mto Tana na eneo la Bondo la Ufa.
Peter Outa Afisa wa habari wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya amesema idadi hiyo inahusu yale tu maeneo ambayo waokoaji wa msalaba mwekundu wamefanikiwa kufika.
Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya imesema mvua kali zitaendelea kunyesha katika kipindi cha wiki mbili zijazo na Wakenya wametakiwa kuchukua tahadhari. Mvua zinazonyesha Kenya zimesababisha hasara kubwa kwa miundo mbinu hasa barabara na madaraja.
Wakati huo huo makamu wa rais wa Kenya William Ruto jana usiku aliitisha kikao cha dharura na maafisa husika kujadili mafurukio ambayo yamekumba maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Ruto amesema serikali itachukua hatua za dharura kutuma misaada ya kibinaadamu kwa waathirika na kuongeza kuwa kuna mpango wa kutafuta suluhisho la muda mrefu ili kuhakikisha mvua hazisababishi hasara kama inavyoshuhudiwa kila mwaka.
 

0 comments:

Post a Comment