Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 11 April 2013

Mpalestina afa shahidi katika gereza la Israel

Mfungwa mwingine wa Kipalestina amekufa shahidi katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya gereza la kuogofya la Nafha huko Israel, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Kufuatia kifo hicho, Wapalestina wanaoshikiliwa mateka katika magereza ya Utawala wa Kizayuni wa Israel waliitisha mgomo kwa lengo la kuwajuilisha walimwengu kuhusu hali yao mbaya inayowakabili. Mapema mwezi huu, Maisara Abu Hamdia, mfungwa mwingine wa Kipalestina alikufa shahidi akiwa ndani ya gereza huko Israel. Mateka wapatao elfu 5 wa Kipalestina wanashikiliwa katika jela za utawala haramu na ghasibu wa Israel. Utawala huo ghasibu unaendelea kutekeleza siasa zake za kimabavu dhidi ya Wapalestina kwa kuwaua na kuwakandamiza raia wasiokuwa na hatia yoyote. Tangu mwaka 1948 hadi hii leo, zaidi ya Wapalestina laki nane na nusu wamekamatwa na kuswekwa katika jela za kutisha za utawala wa Kizayuni. Kuendelea hatua za ukandamizaji za utawala wa Kizayuni dhidi ya mateka wa Kipalestina na udhaifu wa jumuiya za kimataifa katika kufuatilia faili la mateka hao kumezidisha machungu ya wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. Hii ni katika hali ambayo jamii ya kimataifa imeendelea kunyamazia jinai za utawala haramu wa Israel, sambamba na utawala huo ghasibu kuungwa mkono na kusaidiwa na nchi za Magharibi.
 

0 comments:

Post a Comment