Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Iran na Burundi kuimarisha uhusiano

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi mjini Tehran ambapo Ahmadineajd amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili. 
Rais Ahmadinejad amesema mataifa ya Iran na Burundi yana maadui wa pamoja na hivyo yanapaswa kushirikiana katika kukabiliana na maadui.
 Amesema nchi hizi mbili zitashirikiana katika mkondo wa ustawi wa maendeleo na kuondoa umasikini. Rais Ahmadinejad amesema katika uga wa kimataifa, Burundi imekuwa ikitetea haki za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivyo Iran nayo iko pamoja na watu na serikali ya Burundi katika juhudi zao za ustawi na maendeleo. Kwa upande wake Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amesema uhusiano wa Tehran na Bujumbura ni mpana na wenye mikakati. Amesema Burundi daima itakuwa pembeni mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Rais Nkurunziza  amesema mashirika ya Iran yanakaribishwa kuwekeza katika sekta mbali mbali za Burundi. Rais Pierre Nkunruziza wa Burundi, amewasili hapa mjini Tehran leo Jumanne kwa ziara rasmi yenye lengo la kukutana na kufanya viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika safari hii nchi mbili zitatiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano.

0 comments:

Post a Comment