Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Museveni aipongeza Kenya kwa kupuuza ICC

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amelipongeza taifa la Kenya kwa kumchagua Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Nne wa nchi hiyo sambamba na kupuuza vitisho vya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
Akizungumza leo mjini Nairobi katika sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, Rais Museveni amesema kuna watu ambao wanataka kutumia ICC vibaya kwa malengo yao binafsi. Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashtakakatika mahakama hiyo yenye makao yake The Hague kwa tuhuma za kuhusika katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya. Wawili hao wamekanusha tuhuma hizo na kusema watashirikiana na ICC. Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Kiafrika waliohudhuriwa sherehe za kuapishwa Kenyatta katika Uwanja wa Michezo wa Kasarani mjini Nairobi, Museveni amesema, madola yenye kiburi yamepotosha muelekeo wa ICC na sasa yanaitumia mahakama hiyo kuweka viongozi wawatakao Afrika na kuwaondoa wasiowataka. Museveni amesema kuwa, nchi yake imepeleka kesi ya kiongozi wa waasi wa LRA wa Uganda katika mahakama ya ICC kwa sababu waasi hao walifanya jinai nje ya mipaka ya Uganda.  Sherehe za kuapishwa Kenyatta zimehudhuriwa na viongozi wa Mashariki mwa Afrika na viongozi wa nchi muhimu za Afrika kama vile Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Goodluck Jonathan wa Nigeria.
 

0 comments:

Post a Comment