Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 9 April 2013

TCRA yatangaza kiama wanaokiuka sheria ya mawasiliano

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watu watakaobanikia kuvunja Sheria ya Mawasiliano ya Electroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, kwa kushindwa kutimiza vipengele vya sheria hiyo vinavyozuia matumizi na taratibu mbaya za uuzaji na usajili wa namba za simu za mkononi.

Licha ya onyo hilo, mamlaka hiyo imewakumbusha wananchi baadhi ya makosa ambayo hufanyika katika taratibu za uuzaji, utumiaji na usajili wa namba ili wajiepushe na rungu kali litakalowakuta.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa umma jana, iliwataka wananchi kufahamu makosa ambayo hukiuka vipengele vya sheria ya Epoca 2010 katika matumizi na biashara ya namba za simu za mkononi.
Baadhi ya makosa yaliorodheshwa, ni kuuza au kusambaza namba ya simu bila kibali cha mtoa huduma za simu ambaye ana leseni kutoka TCRA; kutumia namba ya simu ambayo haikusajiliwa na kutoa taarifa ya uongo au maelezo yasiyo sahihi wakati wa usajili.
Mengine ni kuchakachua simu ya mkononi au namba na kutoandikisha taarifa zake husika kabla ya kuitoa au kuiuza.
Profesa Nkoma aliwakumbusha watoa huduma wote na wakala wao kuhakikisha wanazingatia kuweka kumbukumbu na taarifa kuhusu wakala wao na kuandikisha watumiaji wanaonunua, au kupatiwa namba za simu.
“Kutotoa taarifa za wateja bila idhini ya mamlaka husika na wauzaji wote waliodhinishwa wana wajibu,” alisema Profesa Nkoma.     


0 comments:

Post a Comment