22,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 03,2013Miyladiyah
kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman
.............................................................
Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya
zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa
vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya kiimani ya nani
achinje kati ya mkristo na Muislam .
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat
anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa
makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa
viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa
wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.
Alisema kuwa kabla ya ijumaa kuu
viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na mkuu wa wilaya ya
Momba Abuud Saibea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya kufanya
hivyo .
Hata hivyo inaelezwa kuwa vurugu
hizo za leo hazina mahusiamo ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani
wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe ambao baadhi
yao wamechanganyika na vibaka kwa lengo la kuchafua hali ya hewa .
Kwani suala la uchinjaji ambalo
lilifanyika siku ya Pasaka halikuwa na mvutano wowote baada ya
wakristo kuchinja katika bucha zao na waislamu hao kuchinja katika
mabucha yao na kila mmoja kufanya biashara kwa kupata wateja wake
kama kawaida .
Ila katika hali ya kushangaza ni baada
ya leo kuibuka kundi hilo la vijana wanaofanya kazi katika stendi
na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati
kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa
wamekusanyika maeneo mbali mbali .
Kutokana na vurugu hizo mpaka wa
Tunduma ambao unaingia nchi za kusini wa Tanzania ulifungwa pamoja
na magari yaliyokuwa yakitoka Sombawanga pia kuzuiwa kuendelea na
safari hadi hali hiyo ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya
kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo hilo.
Taarifa zisizo rasmi ambazo bado
kuthibitishwa na jeshi la polisi zinadai kuwa mtu mmoja ndie
amejeruhiwa japo hakuna madhara makubwa yaliyojitokeza .
====Chanzo cha habari hii ni kwa hisani ya mtandao wa Francis Godwin====
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment