Taarifa ya Jeshi la Uganda imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya serikali ya nchi hiyo kuangukia mikononi mwa waasi wa Muungano wa Seleka. Jeshi la Uganda limesisitiza kwamba, operesheni ya kumsaka Joseph Kony kiongozi wa kundi la waasi wa LRA, makamanda na wapiganaji wa kundi hilo imesimamishwa hadi hapo baadaye.
Tarehe 23 na 24 ya mwezi uliopita, waasi wa Muungano wa Seleka waliingia mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na kuipindua serikali ya Rais Francois Bozize kwa madai ya kukiuka makubaliano ya amani ya Libreville. Imeelezwa kuwa, Bozize alikimbilia nchini Cameroon na ameomba hifadhi nchini Benin.
0 comments:
Post a Comment