27Jumaadal ula,1434 Hijiriyah/ April 08,2013 Miyladiyah
Harakati ya Ukombozi ya Azawad imetangaza kuwa, ingali inasisitiza juu
ya mamlaka ya kujitawala eneo la kaskazini mwa Mali. Viongozi wa
Harakati ya Azawad wamesisitiza juu ya kuweko mazungumzo yenye lengo la
kupatikana amani na kuhitimishwa makumi ya miaka ya kukaliwa kwa mabavu
eneo hilo na serikali kuu ya Mali.
Msimamo huo wa Harakati ya Ukombozi
wa Azawad ni jibu kwa ombi la Laurent Fabius Waziri wa Mashauri ya
Kigeni wa Ufaransa aliyeitaka harakati hiyo iweke chini silaha na iingie
katika mchakato wa kisiasa nchini Mali.
Wakati huo huo, imeelezwa kuwa,
hali ya kibinaadamu nchini Mali inazidi kuwa mbaya. Ripoti zinasema
kuwa, watoto ndio wahanga wakuu wa mapigano na vita vya Mali.
Mfuko wa
Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto wanaokaribia
laki mbili wanakabiliwa na hatari ya kufariki dunia au kujeruhiwa na
milipuko ya mabomu nchini humo. UNICEF imesema kuwa mabomu hayo ambayo
bado hayajalipuka yamesalia nchini Mali tangu mwanzoni mwa mapigano
yanayoendelea sasa kati ya vikosi vya majeshi ya Ufaransa na makundi
yenye silaha katike eneo la kaskazini mwa Mali.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment