Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 7 April 2013

Mkapa: Watanzania jiepusheni na kuvuruga amani


                                    27Jumaadal ula,1434 Hijiriyah/ April 08,2013 Miyladiyah
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaasa Watanzania na vitendo vitakavyopelekea kuvurugika amani ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Mkapa amesema kuwa, taifa la Tanzania linapaswa kujenga utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.
Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea serikali yake kwamba haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.
Matamshi ya Rais Kikwete na mtangulizi wake Mkapa yametolewa katika kipindi hiki ambapo Tanzania imetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini.
Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita. Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja katika mikoa ya Geita na Mbeya.

0 comments:

Post a Comment