Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 9 January 2013

Marekani kutuma ndege zisizo na rubani Kongo

Marekani imesema kuwa iko tayati kutuma ndege zisizo na rubani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kusaidia mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
Marekani imetangaza uamuzi huo baada ya Mkuu wa Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Herve Ladsous kutaka Baraza la Usalama lipanue operesheni za mpango huo nchini Kongo DRC kwa kutumia helikopta nyingi zaidi na ndege zisizo na rubani za usimamizi. Hata hivyo Rwanda imeonyesha wasiwasi kuhusu mpango huo ikisema kwamba itaviorodhosha vikosi vya Umoja wa Mataifa kenye makundi 'yanayotumia mabavu'. Kuna askari 19,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo DRC kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kurejesha amani mashariki mwa nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment